Zijue Faida za vitunguu saumu kwa mwanaume na jinsi ya kutumia
Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.
Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu ( vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.
Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine
mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Kitunguu saumu kina allicin , kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzinguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.
Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.
Namna ya kutumia kitunguu swaumu:
1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
4. Menya punje moja baada ya nyingine
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4.
Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama unmepona tatizo lako. Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, muhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1.
No comments