YANGA: TUMEJIPANGA KURUDI KIGOMA NA KOMBE
KATIKA kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho
la Azam Sports (ASFC), uongozi wa Yanga
kupitia kwa Ofisa Habari wake, Hassan Bumbuli,
umefunguka kuwa wamejipanga vizuri
kuhakikisha wanatwaa ubingwa na kurejea na
kombe la michuano hiyo.
Fainali hiyo inatarajiwa kupigwa leo Julai 25,
Jumapili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,
Kigoma ambapo Yanga watacheza dhidi ya
Simba.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Bumbuli
alisema kuwa Kigoma lengo lao kubwa ni
Kombe la Azam kwa kuwa wamejipanga kupambania ushindi huo.
“Maandalizi yamefikia katika hatua nzuri hadi
sasa timu yetu tayari imeshawasili kigoma ikiwa
na idadi ya wachezaji 20.
“Tumejipanga vizuri kupambana ili kuhakikisha
tunapata ushindi kwa sababu
lengo letu ni kuchukua kombe,” alisema.
Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Simba ambao walitwaa msimu uliopita walipocheza na Namungo katika mchezo wa fainali, Sumbawanga, Uwanja wa Nelson Mandela.
No comments