Breaking News

Walioachiwa kwa msamaha wa Rais wauawakwa tuhuma za wizi



 Watu wawili waliotoka gerezani Aprili 12, Mwaka huu kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.

Wawili hao walifungwa kwa makosa ya wizi katika kesi ya jinai namba 273/2020 na 260/2020 katika gereza la Mkuza mjini Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa, amesema leo Mei 10, 2021 watu hao wameuawa Mei 8 alfajiri kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo na wananchi wenye hasira waliowatuhumu kuhusika kwenye tukio la wizi.

No comments