Breaking News

Tanzania yajizatiti katika mapambano dhidi ya virusi vya corona


Ikulu nchini Tanzania imejizatiti katika kuhakikisha kipimo cha joto na usafi wa mikono wakati nchi inachukua hatua ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Jumatatu, Rais Samia Suluhu alipokea wajumbe wa kigeni ambao wote walitakiwa kuvaa barakoa na picha zilizopigwa wakati huo pia zilionesha rais akiwa amevaa barakoa.

Rais Samia alionekana amevaa barakoa kwa mara ya kwanza akiwa nchini Tanzania alipokuwa anakutana na wazee akisema ni muhimu kuwalinda wazee ambao alikuwa akikutana nao.

Hoja hiyo ilikuwa siku chache baada ya ziara yake Kenya ambako alikuwa amevaa barakoa. Alizungumza kwa utani kwamba kuvaa barakoa kunamkumbusha wakati ule wakiwafunga mdomo mbuzi ili kuwazuia kula mazao ya watu , lakini alisisitiza kuwa ilikuwa jambo la muhimu kuchukua tahadhari.

Rais Samia alitangaza kusudio la kuunda kamati ya wataalamu watakaoshauri juu ya mustakabali wa kukabiliana na corona nchini humo.

Rais Samia alisema Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa katika janga hilo la corona ambalo linaitikisa dunia kwa mwaka mmoja uliopita.

"Suala la Covid 19 nakusudia kuunda kamati ya kitaalamu. Halifai kulinyamazia bila kufanya tafiti ya kitaalamu. Watuambie upeo wa suala hili... Sio ikitajwa Tanzania basi inakuwa deshi, deshi...Hatuwezi kujitenga kama kisiwa," ameeleza Rais Samia.

No comments