Breaking News

SIMBA YAPIGWA 4G NA KAIZER CHIEFS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 


 MBINU za Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba akisaidiana na Kocha Msaidizi Seleman Matola leo Mei 15 zimegonga mwamba mbele ya wapinzani wao Kaizer Chiefs katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fanali ya kwanza kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0.

Ni Eric Mathoto dakika ya 6 alipachika bao la kwanza kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya mabeki wa Simba kushindwa kuweka ulinzi imara kwenye eneo lao la 18 na Samir Nurkovic ambaye alikuwa mwiba leo kwa Simba alipachika bao la pili dakika ya 34 na kuwafanya Simba waende mapumziko wakiwa na mzigo wa mabao mawili.

Ngoma iliendelea kupigwa kwa kasi huku Kaizer Chiefs wakicheza kwa kushambulia kwa kushtukiza huku Simba wakiwa kwenye umiliki na kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza.

Dakika ya 57 chuma cha tatu kilipachikwa na yuleyule aliyewafunga kipindi cha kwanza Nurkovic kwa makosa yaleyale ya mabeki.

Kabla ya mpira kukamilika ni Castro Leonardo Casro ambaye alipachika msumari wa mwisho na kuivunja rekodi ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kuokota mabao mawili pekee kwenye mechi tano ambazo alicheza hatua ya makundi.

Jitihada za Chris Mugalu, Clatous Chama, Luis Miquissone ziligonga mwamba na kufanya timu icheze bila kuwa kwenye hali ya kuleta hatari kwa wapinzani.

Sasa kazi inabaki Mei 22 kwa Simba kusaka ushindi wa mabao matano bila kuruhusu kufungwa ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali.

No comments