Simba kukwea pipa kuifuata Kaizer Chiefs leo
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Gomes amesema kuwa wanatarajia kuondoka leo Jumatatu kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao.
"Jumatatu jioni tunatarajia kuondoka Tanzania kuelekea Afrika Kusini," .
Wachezaji wa Simba watakwea pipa wakiwa na kumbukumbu mbaya ya mchezo wao dhidi ya watani wa jadi Yanga kuyeyuka kutokana na mkanganyiko ulitokea Mei 8.
Mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa saa 11:00 jioni ila Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) lilitoa taarifa kwamba utachezwa majira ya saa 1:00 usiku jambo ambalo liligomewa na Yanga kwa kueleza kuwa ni kinyume na kanuni.
Kwa sasa TFF wameeleza kuwa wanalifanyia kazi suala hilo ili kujua hatma ya mchezo huo ambao umesababisha hasara kubwa na inakuwa ni rekodi ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni kutokea.
No comments