Breaking News

Serikali yaombwa kuingilia kati kesiya mtoto aliyebakwa akiwa na miaka 3 na kushindwa mahakamani


Wananchi wa mtaa wa Mpeto kata ya Ramadhani mjini Njombe,wameiomba Serikali kuingilia kati kesi ya mtoto wa mtaa huo aliyebakwa akiwa na umri wa miaka 3 mwaka 2018 na kusababishiwa maumivu makali pamoja na kutafutiwa njia mbadala kwa ajili ya haja kubwa na ndogo huku mjomba wake aliyetuhumiwa na kesi hiyo kushinda Mahakamani.

Aidha wameomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaume wabakaji na walawiti wa watoto na kuwasababishia ulemavu kufuatia wahusika waliowengi wa matukio hayo ya kikatili kushikiliwa kwa muda na kisha kuachiwa bila kufanywa chochote.

Hayo  yamebainishwa na wananchi hao walipojitekeza katika ofisi ya mtaa huo  kuchangia mtoto wa kike aliyefanyiwa kitendo cha ubakaji  mwaka 2018  na kupata ulemavu ambao unagharimu fedha nyingi kwaajili ya matibabu katika hospitali ya taifa ya Mhimbili.

“Kwasababu wananchi tumekusanyika hapa kwa maana hiyo jambo hili linafahamika kiserikali,kwa hiyo jambo langi la kwanza nitoe rai kwa vyombo vyote vya serikali juu ya hili swala kwasababu sisi tumeonyesha njia kuwa kuna jambo huku na mtoto anahitaji msaada”alisema Alex Mwalongo mkazi wa mtaa huo

 

No comments