Breaking News

Samia Suluhu: Imekuwa ni vigumu kwangu kuongeza mshahara

 

I

CHANZO CHA PICHA,MAELEZO

Katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani nchini Tanzania , Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan amesema licha ya matamanio yake ya kuongeza mishahara lakini inamuwia vigumu kufanya hivyo kwa sasa.

Alianza kusema "Ndugu zangu mimi ni mama na mama ni mlezi ila kuna msemo usemao kuwa masikini huwa anapenda mwanae apendeze lakini shida ni uwezo."

Rais Samia amesema ameshindwa kutimiza matamanio ya wafanyakazi mwaka huu kwa kuwa kasi ya uchumi imeshuka na kwa Tanzania uchumi umeshuka kutoka asilimia 6.9 mpaka asilimia 4.7 na hii inatokana na mlipuko wa janga la corona.

Lakini amehaidi kupunguza kodi na tozo mbalimbali za serikali kwa wafanyakazi. Aidha imemuwia vigumu kuongeza mshahara kwa kuwa ndio kwanza anaanza kazi lakini mwakani ataweza kutimiza dai hilo ambalo ni mhimu kwa wafanyakazi.

No comments