Breaking News

Panya 'kupima' corona Tanzania



Watafiti nchini Tanzania kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa panya kutumika kutambua maambukizi ya virusi vya corona, Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini humo.

Dkt.Georgies Mgode, mtafifiti kutoka SUA ameliambia gazeti hilo kuwa wana imani kuwa panya wanaweza kutambua virusi vya corona kwa ufanisi mkubwa kwa sababu tayari wameona mafanikio ya jinsi panya wanavyoweza kutambua mabomu yaliyojificha ardhini na kutambua vimelea vya kifua kikuu.

"Vipimo vya virusi vya corona kwa sasa ni ghali na vinatoka nje ya nchi, lakini kwa kutumia panya itakuwa rahisi na itapunguza maumivu kwa wanaopimwa kwa vifaa."

Vilevile gazeti hilo limemnukuu Dkt.Mgode akisisitiza kuwa kutambua maaambukizi ni jambo muhimu kwani kutasaidi kujilinda na wale watakaokutwa na maambukizi kupata huduma kwa haraka hivyo kupunguza vifo na maambukizi.

Ameishukuru serikali kwa kuruhusu matumizi ya panya katika hospitali zake kwa makubaliano kuwa majibu yathibitishwe na teknolojia nyingine zinazokubalika kabla majibu hayatumika hospitalini.

No comments