Breaking News

ORODHA YA WACHEZAJI WA SIMBA WALIOPO NCHINI AFRIKA KUSINI

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes jana Mei 11 kiliwasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.

Mchezo huo ambao ni robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Mei 15 nchini Afrika Kusini.

Tayari kwa sasa kikosi kimeanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho na  hii hapa ni orodha kamili ya msafara wa wachezaji ambao kwa sasa wapo nchini Afrika Kusini ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Chris Mugalu, Ibrahim Ame.

 Meddie Kagere, Mzamiru Yassin, Fracis Kahata, David Kameta.

Wengine ni Gadiel Michael, Kenedy Juma, Pascal Wawa, Clatous Chama, Taddeo Lwanga, Larry Bwalya, Hassan Dilunga, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Joash Onyango, John Bocco na Luis Miquissone.

No comments