Breaking News

Marekani imepitisha sheria ya dharura baada ya kuvamiwa kimtandao kwa bomba la mafuta


Colonial Pipeline in Georgia

CHANZO CHA PICHA,COLONIAL PIPELINE

Serikali ya Marekani imepitisha sheria ya dharura siku ya Jumapili baada ya bomba kubwa la mafuta la nchini humo kushambuliwa kimtandao na genge la wahalifu linalotaka malipo.

Bomba hilo kwa kina la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku - sawa na 45% ya mahitaji ya mafuta ya Pwani ya Mashariki nchi hiyo na liinasambaza mafuta ya dizeli, ya petroli na mafuta ya ndege.

Wahalifu wa mtandaoni walifanya hujuma dhidi ya bomba ambalo limeshindwa kushindwa kufanya kazi tangu siku ya Ijumaa na mpaka sasa bado oparesheni ya kujaribu kurudisha huduma za bomba hilo zinaendelea.

Hali ya dharura inaruhusu mafuta kusafirishwa kwa njia ya barabara.

Jumla ya majimbo 18 yamepewa muda kidogo kusafirisha mafuta ya petroli, dizeli, ya ndege na aina nyingine za bidhaa za mafuta.

Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Columbia, Delaware, Florida, Georgia, Kentucky, Louisiana, Maryland, Mississippi, New Jersey, New York, North Carolina, Pennsylvania, South Carolina, Tennessee, Texas na Virginia.

Wataaamu wanasema bei ya mafuta inaweza kuongezeka kwa asilimia mbili mpaka tatu leo Jumatatu, lakini athari zitakuwa kubwa zaidi kama tatizo hili litaendelea zaidi ya Jumatatu.

Mchambuzi huru wawa soko la mafuta Gaurav Sharma ameiambia BBC kuwa kuna shehena kubwa ya mafuta iliyokwama kwenye vituo vya kusafishia mafuta huko Texas.

"Labda kama wataweza kutatua tatizo hilo ifikapo Jumanne, ila wapo kwenye tatizo kubwa," alisema bwana Sharma. "Maeneo ya kwanza ambayo yatapata athari yanaweza kuwa ni Atlanta na Tennessee, na athari inaweza kufika New York."

Alisema wafanyabiashara wa mafuta wanahangaika sasa ili kufikia mahitaji ya watu kwa wakati, wakati hesabu ikipungua na mahitaji haswa ya mafuta ya magari yakiongezeka baada ya watumiaji wengi kuwa wamerudi barabarani na uchumi wa Marekani ukiwa unajaribu kurudi juu baada ya athari za janga la corona.

The Colonial Pipeline

CHANZO CHA PICHA,COLONIAL PIPELINE

Maelezo ya picha,

Bomba hilo la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku

Sheria hiyo ya msamaha ya muda iliyotolewa na idara ya usafirishaji inawezesha bidhaa za mafuta kusafirishwa kwa meli mpaka New York, lakini haitasaidia kwa namna yeyote kukidhi mahitaji ya bomba hilo la mafuta, bwana Sharma alitoa angalizo.

Vyanzo kadhaa vimethibitisha kuwa shambulio hilo la kimtandao lilifanywa na genge la wahalifu wanaofahamika kama DarkSide, ambao walivamia mtandao wa bomba la mafuta la kikoloni siku ya Alhamisi na kuchukua karibu 100GB za data la bomba hilo.

Baada ya kuchukua data hizo,wavamizi wa mtandao walifunga data za baadhi ya komputa na kutaka malipo siku ya Ijumaa.

Lakini malipo hayo yasipotolewa, wametishia kuvujisha kwenye intaneti.

Colonial imesema inafanya kazi na sheria iliyowekwa, wataalamu wa usalama wa mtandaoni na idara ya nishati ili kurudisha huduma hiyo.

Jumapili jioni ilisema licha ya kuwa njia nne kuu zimezimwa, kuna njia nyingine ndogo kutoka eneo moja mpaka sehemu ya kupokelea mizigo ambayo inafanya kazi.

"Mara tu baada ya kubaini shambulio hilo, Colonial iliamua kuzima mifumo mingine kama tahadhari la tishio.

Hatua hii iliatiri kwa muda utendaji wa bomba hilo na kuathiri mfumo wa taarifa ambao ulikuwa unarudisha huduma," kampuni hiyo imeeleza.

"Tuko kwenye jitihada za kurejesha mifumo yote mtandaoni pale ambapo tutaamini kuwa ni salama na kudhibitishwa na mamlaka zote za shirikisho."

An example of a DarkSide ransomware notice that appears on victims' computer screens
Maelezo ya picha,

Wadukuzi hao waliacha maandishi kama hayo kwenye komputa walizofanya udukuzi

Wakati wadukuzi hao wa DarkSide sio genge kubwa katika eneo hilo lakini tukio hilo linaongeza hatari ya kuadhiri miundombinu ya taifa viwanda na sio biashara peke yake.

Vilevile inaashiria kuongezeka kwa mfumo wa uhalifu wa kihalifu katika mfumo wa teknolojia ambao una thamani ya mamilioni ya pauni, ambayo ni tofauti na kitu chochote ambacho sekta viwanda ya usalama wa mtandao imewahi kukukabiliana nayo.

Ukiachana na ilani iliyoachwa kwenye komputa , waathirika wa shambulio la DarkSide wamepokea kifurushi cha habari kuwajulisha kuwa kompyuta na mifumo yao imedukuliwa.

Genge hilo limeorodhesha aina zote za data ambazo wameiba na kuwatumia waathirika kurasa binafsi ambayo ilivujishwa ambapo tayari data ilikuwa inachukuliwa na kusubiri kujichapisha yenyewe,hivyo kampuni inapaswa kulipa kabla ya muda waliopewa kufika.

DarkSide waliwaambia waathirika pia kuwa watatoa ushahidi wa data ambazo wako nazo na wanajiandaa kufuta zote katika mtandao wa wahanga wao.

Kwa mujibu wa Digital Shadows, kampuni ya uslama wa mtandaoni iliyopo inafuatilia wadukuzi wa mtandao ili kusaidia makampuni kutodukuliwa mtandaoni , DarkSide inafanya kazi kama biashara.

Genge hilo linafanya kazi kwa kuwa na mfumo ambao unaiba data ambayo inawashirikisha washirika kwa kutuma barua pepe ya kutaka jambo na namna ya kufanya shambulio.

Washirika wa genge la wadukuzi wa mtandaoni wanawalipa DarkSide asilimia kadhaa ya kile ambacho watakipata kwa shambulio lolote ambalo litafanikiwa.

Na kuachiwa kwa mfumo mpya mwezi Machi inaweza kuhifadhi data haraka zaii kabla ya genge la wahalifu alijatoa taarifa kwa vyombo vya habari au kuwaalika wageni kwa ajili ya mahojiano.

No comments