Breaking News

Mahakama yaifuta kesi ya kina Halima Mdee na wenzake

 

 


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru viongozi na wafuasi 27 wa Chadema waliokuwa wanadaiwa kufanya mkusanyiko na kuvunja geti la gereza la Segerea chini ya kifungu cha 225(5) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA.)

Kesi hiyo imefutwa leo Mei 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi mahakamani.

No comments