Breaking News

Kwanini mataifa ya Afrika hayaikosoi China kwa kuwanyanyasa Waislamu wa Uyghurs

 


Mataifa ya Afrika hakuunga mkono hatua ya Umoja wa Matifa kukashifu ukiukaji wa haki za binadamu wa taifa hilo

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Mataifa ya Afrika hayakuunga mkono hatua ya Umoja wa Matifa kukashifu ukiukaji wa haki za binadamu wa taifa hilo

Mataifa ya Afrika sio miongoni ma mataifa yanayoshutumu vitendo vya China dhidi ya Waislamu wa kabila la Uyghur katika jimbo la kaskazini magharibi la Xinjiang.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba hivi majuzi wanadiplomasia walikwenda mjini Beijing na kuisifu China kuhusu sera yake katika eneo hilo.

Takriban Waislamu milioni moja wa kabila la Uyghurs wanaaminika kuzuiliwa katika eneo la Xinjiang katika msururu wa kambi.

China inakabiliwa na shutuma za kuwalazimu, mateso na mauaji ya kimbari - madai ambayo imekanusha.


Serikali ya China imetetea kitendo chake cha kuwazuia Waislamu katika kambi, ikidai kwamba ni taasisi za mafunzo ya kukabiliana na ugaidi na itikadi kali za kidini.

''Baadhi ya mataifa ya magharibi yanatumia suala hilo la Xinjiang kuishambulia China ili kupigania maslahi yao, Adama Compaore'' , balozi wa Burkina fasso , alinukuliwa akisema katika hafla moja mwezi Machi kwa jina Xinjiang kulingana na mabalozi wa Afrika.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Sudan na Congo Brazzaville , ambaye balozi wake Daniel Owassa aliripotiwa akisema kwamba aliunga mkono kile ambacho China imekitaja msururu wa mikakati ya kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo akisema kwamba anaunga mkono hatua za maenedeleo zilizopigwa Xinjiang katika sekta mbalimbali katika miaka ya hivi majuzi.

Shirika la haki za kibinadamu la Humans Rights Watch HRW lilisema kwamba mkutano huo ulikuwa mfano wa kunyamaza kwa Afrika kuhusu masuala tata yanyaoendelea duniani.

Mabadiliko ya kizazi?

Ejeviome Otobo, katika taasisi ya utawala ya Global Governance Institute mjini Brussels, anasema kwamba viongozi wa Afrika na China wanauelewa wa kufanana , katika masuala matatu tofauti: Haki za Binadamu, Maslahi ya kiuchumi na kutoingilia masuala ya ndani ya nchi.

Uungwaji mkono wa Afrika kwa China unaoongezeka kila uchao unalifanya bara hili kutengwa na bara Ulaya inapokuja katika masuala ya haki za kibinadamu.

Wakati wa uchaguzi mwezi Juni 2020 katika baraza la haki za binadamu huko Geneva kuhusu suala tata la sheria ya usalama wa kitaifa wa Hong Kong , ambayo iliweka adhabu kali kuhusu wapinzani wa kisiasa na ambayo ilimaliza kujitawala kwa eneo hilo , mataifa 25 ya Afrika , ikiwa ni kundi kubwa zaidi, liliunga mkono China.

Miezi kadha baadaye,mwezi Oktoba hakuna taifa lolote la Afrika liliotia saini makubaliano ya kuishutumu China kwa kukiuka haki za kibinadamu za Xinjiang , Hong Kong na Tibet makubaliano yalioungwa mkono na mataifa ya magharibi.

HRW linawashutumu viongozi wa Afrika kwa kupatia kipaumbele faida zao za kiuchumi kutoka kwa China na kutupilia mbali utata uliopo.

Eric Olander, mwanzilishi wa mradi wa China na Afrika anasema kwamba kwa hatua ya watengenezaji wa sera za Afrika kutoipinga China ni sera muhimu ya kigeni .

Kile ambacho wakosoaji hao hawaelewi ni kwamba kama mataifa maskini yanayoendelea - mengi yakiwa yana madeni ya Beijing na hutegemea China kwa biashara nyingi hayapo tayari kuhimili athari za kuikasirisha China, aliambia BBC.

China hufanya mkutano na mataifa ya Afrika Kila baada ya miaka mitatu

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

China hufanya mkutano na mataifa ya Afrika Kila baada ya miaka mitatu

Suala jingine ni uhusiano wa miongo kadhaa uliowekwa mwaka 1970 wakati mataifa ya Afrika yalipochukua jukumu muhimu katika kuisadia China kujiunga tena na Umoja wa mataifa licha ya pingamizi kutoka kwa Marekani..

"Tangu wakati huo , uhusiano umeimarika, Cliff Mboya mchambuzi wa masuala ya China na Afrika aliambia BBC.

"Kwa miaka 30 sasa China imefanya utamaduni kwamba waziri wake wa masuala ya kigeni anatembelea Afrika kila mwaka - hiyo sio tu ishara bali inaonyesha jinsi taifa hilo lilivyowekeza katika uhusiano wa muda mrefu na huo ni muonekana mzuri kwa Waafrika."

Waafrika vijana huenda hawavutiwi -huenda wanapendelea sana Marekani na mtindo wake wa maendeleo kulingana na Utafiti wa hivi majuzi uliofanywa na Afrobarometer.

Lakini watu wenye umri mkubwa na viongozi wa serikali wanahisi tofauti na uamuzi wao wa kuelekea China kwa ufadhili wa miundo msingi hususan katika kipindi cha miaka 20 umebadilisha mandhari ya Afrika kupitia barabara za hali ya juu , madaraja, reli ya kisasa , bandari na miundo mbinu ya intaneti ambayo imehakikisha kuwa bara hili halijatengwa katika uchumi wa Kidijitali.

Chanjo ya China imekuwa ikitumiwa nchini Zimbabwe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Chanjo ya China imekuwa ikitumiwa nchini Zimbabwe

Diplomasia ya Chanjo

Tangu mlipuko wa virusi vya corona ulipozuka , Bendera za China zimekuwa zikionekana mara kwa mara katika viwanja vya ndege katika bara la Afrika ikiwa ni ishara ya kuwasili kwa ufadhili kama vile vifaa vya kujilinda dhidi ya corona na hivi karibuni Chanjo zilizotengenezwa kutoka China.

Diplomasia ya Chanjo za China imefikia mataifa 13 barani Afrika ambayo yamezinunua ama hata kupata kama ufadhili.

Barabara ya Nairobi ya juu kwa juu inayojengwa ni miongoni mwa miradi iliofadhiliwa na China

CHANZO CHA PICHA,BB/PETER NJOROGE

Maelezo ya picha,

Barabara ya Nairobi ya juu kwa juu inayojengwa ni miongoni mwa miradi iliofadhiliwa na China

Ikiliganishwa hakuna hata ufadhili wa moja kwa moja kutoka Uingereza ama Marekani isipokuwa kupitia mpango wa Covax duniani ambao pia unasaidiwa na China.

Covax imetoa chanjo milioni 18 duniani kufikia sasa katika mataifa 41 barani Afrika.

Matumizi ya Chanjo yametumiwa kama chombo cha ushawishi ulimwenguni kati ya mataifa yenye uwezo mkubwa duniani.

No comments