Breaking News

Fahamu umuhimu wa msikiti wa Al-Aqsa ulio katikati ya ghasia Jerusalem

 


Msikiti wa Al-Aqsa Jerusalem

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Msikiti wa Al-Aqsa Jerusalem

Takriban Wapalestina 300 na maafisa sita wa Israel wamejeruhiwa katika ghasia mjini Jerusalem , kulingana na madaktari wa Palestina na polisi wa Israel.

Wengi wao walijeruhiwa katika msikiti wa Al-Aqsa, ambapo maafisa wa polisi wa Israel walirusha risasi bandia na maguruneti huku Wapalestina wakirusha mawe na chupa.

Msikiti wa Al -Aqsa , mmoja wa maeneo matakatifu ya Waislamu ni tofauti na misikiti mingine.

Hizi hapa sababu tatu kuhusu umuhimu wa msikiti huo na mji wa Jerusalem kwa jumla.

1.Kwanini msikiti wa Al- Aqsa ni muhimu?

Al-Aqsa ni jina la msikiti uliopo katika ardhi yenye ekari 35 na hufahamika na Waislamu kama al-Haram al-Sharif, huku Wayahusi wakiuita Hekalu.

Msikiti huo usio wa kawaida upo mjini Jerusalem na ni eneo ambalo limeorodheshwa miongoni mwa turathi za kitaifa na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu utamaduni UNESCO.

Eneo la msikiti huo ndilo lenye utata zaidi duniani tangu 1967 wakati Israel ilipokalia eneo la mashariki mwa Jerusalem ikiwemo eneo la zamani la mji huo.

Mgogoro huo ulianza zama za kale kabla ya kuzaliwa kwa taifa la Israel.

Msikiti wa Al-aqsa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mwaka 1947, Umoja wa Mataifa ulianzisha mpango wa kuitenga Palestina , wakati huo ikiwa chini ya utawala wa Uingereza, iwe majimbo mawili: Moja la Wayahudi hususan kutoka bara Ulaya na jingine la Wapalestina.

Jimbo hilo la Wayahudi lilipatiwa asilimia 55 ya ardhi huku asilimia ikipatiwa Wapalestina 45 .

Jerusalem inayomiliki eneo la msikiti Aqsa linalimikiwa na jamii ya kimataifa chini ya usimamizi wa UN .

Ilipewa hadhi maalum kutokana na umuhimu wake kwa dini tatu.

Vita vya kwanza kati ya Waarabu na Waisraeli vilizuka 1948 baada ya Israel kutangaza taifa lake , likinyakua asilimia 78 la ardhi ya Wapalestina, huku maeneo yaliosalia ya West Bank , Jerusalem mashariki na ukanda wa Gaza yakidhibitiwa na Misri na Jordan.

Unyakuzi wa Israel katika ardhi ya Wapelestina uliendelea 1967, baada ya vita vya pili vya Arab-Israel ambavyo vilisababisha Israel kukalia eneo la mashriki mwa Jerusalem, kabla ya kuunyakua mji wa Jerusalem, ikiwemo ule wa zamani na al-Aqsa.

Mwaka 1980, Israel ilipitisha sheria ikitangaza kuuteka mji wa Jerusalem kinyume na sheria ya kimataifa.

Hadi kufikia leo, hakuna taifa linalotambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, isipokuwa Marekani chini ya uongozi wa Donald Trump ambaye alihamisha ubalozi wake hadi katika mji huo.

Wapalestina 400,000 wanaoishi Jerusalem wana haki kuishi lakini hawatambuliwa kama wananchi.

Tangu 1967, Israel imekuwa ikiwafurusha Wapalestina kwenda Jerusalem kwa kuwaekea masharti magumu.

Israel imejenga nyumba mjini Jerusalem ambazo ni nyumbani kwa Wayahudi 200,000.

Waislamu wakipinga uamuzi wa Trump mjini Jerusalem

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

2. Umuhimu wa kidini wa Msikiti wa al-Aqsa

Kwa Waislamu , msikiti wa al-Aqsa uliopo mjini Jerusalem ndio eneo la tatu kwa utakatifu.

Msikiti wa Al Aqsa ndio uliokuwa ukitumiwa kama qibla{Eneo ambalo Waislamu hutazama wanaposali} kwanza kabla ya kibla kwenda Mecca.

Ukarabati wa jengo hilo uliofanyika katika karne ya 7 , unaaminika na Waislamu kuwa eneo ambalo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.

Wayahudi wanaamini kwamba jengo hilo takatifu , mara ya kwanza lilikuwa hekalu lao, lakini sheria ya Kiyahudi inapinga kuingia na kuomba kwa kuwa ni eneo takatifu sana.

Ukuta ulioko magharibi mwa msikiti huo unajulikana na Wayahudi kama ukuta wa maombolezo, unaodaiwa kuwa ukuta uliosalia wa hekalu hilo la Wayahudi.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Lakini Waislamu wanaamini kwamba ukuta huo ni ukuta wa Al- Burqa, eneo ambalo mtume Muhammed alifunga al- Buraq wakati alipopaa mbinguni ili kuongea na Mungu.

Ni mwaka 2017 wakati rais Donald Trump wa Marekani alipotangaza kwamba atatambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel hatua ambayo ilipingwa na mataifa mengi ya Kiislamu.

3. Awamu za mzozo huo

Mwaka 1967, Jordan na Israel zilikubaliana kwamba Waislamu watadhibiti eneo la ndani la ndani msikiti huo na ukarabati wake , huku Israel ikidhibiti usalama wa nje wa al-Aqsa.

Wasio Waislamu huruhusiwa kutembelea eneo hilo kwa saa kadhaa lakini hawaruhusiwi kufanya ibada ndani yake.

Lakini mashirika yanayopigania eneo hilo kuwa hekalu la Wayahudi , kama vile hekalu la Mount faithful na lile la hekalu la Institute, wamekuwa wakishinikiza serikali ya Israel kuwaruhusu Wayahudi kuingia katika jumba hilo na wanataka hekalu la tatu kujengwa katika eneo hilo.

Mwaka 2000, waziri mkuu Ariel Sharon aliingia katika eneo la msikiti huo na maafisa 1000 wa polisi.

Kuingia kwa Sharon kulisababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 3000 na Waisraeli 1000.

Watu wakiingia katika msikiti wa Al-Aqsa

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Watu wakiingia katika msikiti wa Al-Aqsa

Israel imeweka vikwazo kadhaa karibu la lango la msikiti wa al-Aqsa , ikiwemo ukuta uliowekwa mwaka 2000, unaowazuia Wapalestina kutoka West bank kuingia.

Kati ya Wapalestina milioni 3 katika eneo la West Bank ni wale walio zaidi ya umri wa miaka 40 wanaoruhusiwa kuingia Jerusalem siku ya Ijumaa huku wengine wakipatiwa sharti la kuwasilisha ombi la kibali kutoka kwa mamlaka ya Israel.

No comments