Breaking News

Athari za kutoongezwa kwa mishahara

 



Kutoongezwa kwa mishahara ya wafanyakazi kumesababisha athari mbalimbali katika sekta tofuti nchini .

Mfano imepelekea kushuka kwa morali ya wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii.

Imewafanya baadhi ya watendaji wa serikali kuacha kazi kutokana na ujira hafifu.

Imesababisha kiwango cha ubunifu katika utendaji wa shughuli za kiserikali kushuka kwa kasi kubwa.

Imeshusha ufanisi wa utendaji wa wafanyakazi ndani ya Serikali kuwa ni wa kusuasua sana kiasi kwamba matokeo ya utendaji wao ndani ya Serikali kuonekana siyo wa kuridhisha kabisa.



Katika kuboresha utendaji wa Serikali ni muhimu maslahi ya watendaji wa Serikali yaani mishahara kuboreshwa kama maadai yao yanavyoainisha na vyama vyao vya wafanyakazi kama vile; TUCTA, RAAWU, CWT, CHODAWU, TUICO, JT, TAMICO, TALGWU na TUGHE, kwani kwa kutokufanya hivyo kunapelekea baadhi ya mambo ya kiserikali kufanyika katika viwango hafifu na visivyo vya kuridhisha hata kidogo.


No comments